Monday, June 22, 2015

SOMO: HAZINA ILIYOFICHWA NDANI YA MBEGU YA NENO LA MUNGU

Pastor Frank Andrea akifundisha katika ibada ya Ufufuo na Uzima Arusha






UTANGULIZI

Isaya 45:1-3

Mungu anasema nitakwenda mbele yako naminitakupa hazina za gizana na mali zilizo fichwa za mahali pa siri. Kuna vitu vipo vimefichwa za mahari pa siri ambavyo Bwana anahaidi atatupatia, Ni muhimu kujua kunavitu vipo ambavyo havionekani lakini Mungu amekuandalia wewe. Hata wakati wa uumbaji kunavitu Mungu alkuwa anavitaja lakini havikuako, Mwanzo 1:1-2, Mungu aliumba dunia na vyote kwa Neno. Kwa maneno mengine ukivichukua vitu vyote na kuviludisha viliko toka vitarudi ndani ya Neno la Mungu. Kitabu cha Yohana 1:1-5 kinasema vitu vyote viliubwa kwa Neno na Ndani ya huyo Neno ndimo mlimokuwepo uzima,,
Neno ni nini?
Kwenye maandiko Matakatifu yaani Bilblia emeeleza Neno kwa namna mbili
       i.            YESU
     ii.            MBEGU

NENO KWA MAANA YA YESU
YESU ni Neno Yohana1:1-4. Neno lilikuwa kinywani mwa MUNGU. Ukikusanya vituvyote virudi kwenye hasiri yake vyote vitarudi kwenye Neno. Huyu Neno kazi yake ilikuwa ni kumtia nuru kila mmoja ulimwenguni. Yohana1:14 inasema naye Neno akavaa mwili tukauona utukufu wake kama wa mwana pekee wa Mungu ambaye alikuwa ni Yesu.
NENO KWA MAANA YA MBEGU
Kitabu Luka 8:11 kinaeleza vizuri kuwa mbegu ni Neno la Mungu. kwa maneno mengine unaweza kusema ndani ya Mbegu ndimo mlimokuwepo uzima. Kwa mfano ukiwa na mbegu ya parachichi ndani yake kuna mapori ya maparachichi. Ukiwa na mbegu ya mchungwa ndani yake kuna mapori ya michungwa. Iliuendane na Mungu lazima ujifunze kuona kama yeye anavyoona..
Utaona Yesu anatoa mfano wa mbegu Luka 8:4-8, Yesu alikuwa anazungumzia Mbegu kama neno la Mungu na mahari pa kupanda kama aina za mioyo ya watu ambao wanalisikia Neno la Mungu.  Aina za mahari pa kupanda mbegu
       i.            Njiani : moyo njia ni moyo ambao mtu analisikia Neno la Mungu lakini  anafungua moyo wake na kuruhusu mambo mabaya kuingia kwake. Na ndege huja kuula
     ii.            Mwamba: moyo mwamba ni moyo usio tayari kupokea chochote, ulisikiliza Neno lakini hulizuia lisiingie ndani yake.
  iii.            Udongo wa Miiba: moyo miiba ni moyo buzy, moyo ambao unasongwa na mambo mengi ya duniani, kama kazi, maisha n.k
  iv.            Udongo mzuri:mbegu iliyo dondoka kwenye udongo mzuri, ni mbegu ambayo imeanguka kwenye moyo mzuri ambao upo tayari kulipokea neno la Mungu na kulitendea kazi, hasa kuzaa watu katika ufalme wa Mungu.
Kunamambo mengina Unaweza kupanda kwa roho yako na kwa mwili;- kuna vitu unavipata au unapanda katika roho unapo sikiliza Neno la Mungu. Kupanda kwa mwili;- kunamatendo ya mwili unayafanya ambayo hayana faida kwenye roho yako. mwanzo 2:7 mwili wa mwana damu ni mavumbi ya aridhi kwa maana yake unaweza kupanda jambo na likaota kwenye mwili. Ndio maana Mungu alimwambia shetani utakula mavimbi ya ardhi ndio maana ni rahisi kwa shetani kupanda magonjwa kwenye mwili wako.
Mwanzo1:12 miche na itoe mbegu, ambazo mbegu zake zimo ndani. Maana yake ndani ya mbegu moja kuna mapori. Mfano mzuri utaona kwa wakulima wanapanda mbegu moja lakini wana vuna muhindi ambao unapunje elfu moja. Je mtu angekula ile punje ya muhindi, maana yake amekula magunia ya mahindi.
MFANO WA MTUNZA MBEGU KAMA NENO LA MUNGU
Utaona katika Biblia kuna watu ambao Mungu aliwajua toka tumboni na kumwambia Raheli mataifa makubwa mawili yanapigana ndani yako. Mwanzo 25:21- 34 mataifa mawili ndani ya tumbo moja, baadaye walizaliwa kwake watoto mapacha, Yakobo na Essau. Yakobo alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anatunza mbegu. Lakini Esau alikuwa ni mwindaji na alikuwa hana uwezo wa kuifazi mbegu, kwasababu  alikuwa akiwinda kwa mshale na kummaliza mnyama. Yakobo alikuwa mkulima ndio maana alikuwa ana tunza mbegu. Utaona kwenye maandiko Essau aliamua kuuza uzaliwa wake wa kwanza kwasababu alikuwa atunzi mbegu kwenye ghala yake. Hakasahau kuwa kuna Baraka ya kuwa mzariwa wa kwanza.  Kwenye Biblia kuna Baraka nyingi za mzariwa wa kwanza lakini kubwa ni hizi:-
BARAKA YA MZALIWA WA KWANZA
                   i.            Baraka ya mzazi
                 ii.            Baraka ya Mungu: Mungu anasema mtoto wa kwanza ni wa Kwangu.
              iii.            Ni mtawala wa familia.
Hatakama umezaliwa maskini ila kwa Baraka za Mungu utafanikiwa.
Essau na Yakobo nani alikuwa Mwizi?
Essau alimwambia Yakobo umeniibia Baraka zangu za uzaliwa wa kwanza, amesahau kwamba alimuuzia uzaliwa wake wa kwanza kwa Yakobo. Kwa maneno mengine kwenye ulimwengu waroho Yakobo alikuwa Essau na Essau alikuwa ni Yakobo. Ndio maana kila mahari Yakobo alipo kwenda alifanikiwa, alipo kuwa kwa Labani alipokuwa anafuga wanyama na wakazaliana sana. Siri ya Yakobo alikuwa anatunza mbegu.
MANENO KAMA MBEGU
Neno la Mungu ni mbegu. Hata maneno ya shetani ni mbegu. Kuna maneno ambayo unajitamkia mwenyewe mabaya yanakuwa ni mbegu kwenye maisha yako. Ndio maana akasema kwenye kitabu cha Yoeri aliye zaifu na aseme mimi ni hodari.
Kanuni ya mbegu ni lazima ioze kabla haija tokea. Maandiko yanasema mbegu isipo anguka chini ya aridhi ikafa haiwezi kumea. Unapo panda mbegu kuna kipindi cha kuishi kwa imani. Kwa mfano ukipanda karanga na kufukia, watu hawata jua hatakama Utaendelea kumwagilia kwasababu ipo chini ya aridhi, lakini unapo zidi kumwagiria ndipo utakapo una imetokea au kuchanua. Lakini wapo wengine wakimwagia wasipoona kitu na hukata tamaa kwa sababu hajaona kitu kinacho onekana pale. Unapo panda mbegu kanuni ya imani inaanza kutumika. Nikama mchungaji akisema poke Biashara kubwa, uanze kuona umepokea kama mbegu. Na uanze kutengeneza picha na kumshukuru BWANA na BWANA atakuinua 2wakorintho4:7 utu wetu wanje unachakaa la kini wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Ishi kwa imani leo ilikesho ukavune. Kunawatu wanakuzalau leo ilakesho watakueshimu kwa jina la YESU. Muhubiri 11:1-6, paangukiapo ule mti papohapo utalala; imani yako inaangukia wapi? Sitakufa bali nitaishi,  anasema asubuhi panda wala usiuzuie mkono wako, wewe panda kila unachokiona baada ya muda utakiona kile ulicho kipanda. Asubuhi panda, jioni panda, usiku panda. Panda kwenye uongozi, utajiri, mifugo, mali na hazina.  Unapokuwa na mbegu usione kama umeshika mbegu ona kama umebeba mapori ya iyo mbegu. Muhubiri 4:14
Unapo panda ukiona mche umetokea anza kuweka na walinzi wa kulinda maana biashara yako, kazi yako, maisha yako yanaenda kuwa mti mkubwa. Kama unacheleani moja anzakuona unachuo cha ushonaji. BWANA akamwambia Abrahimu inua macho yako kuanzia hapo ulipo nchi uonayo nimekupa. Mungu anataka kukutoa kutokea hapo ulipo,, hauwezikuishia hapo kwa jina la Yesu anza kuona ushindi mbele yako kwa Jina la Yesu. Je unaona nini mbele yako leo? Unaona mbegu au unaona pori? Unambegu ndani yako Mungu kaiweka unatakiwa uimwagilie kwa jina la Yesu. Mungu anasema inua macho yako tazama kutokea hapo ulipo anza kuangalia unapo kwenda kwa jina la Yesu
 Watu wanapo kuona maisha yako wana comment maisha yako unayo ishi leo, lakini Bwana anampango mpya na wewe. Heri apandaye kwa machozi atavuna kwa furaha.
Maombi
Baba Mungu katika jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai,Napanda ushindi juu ya maisha yangu kwa jina la Yesu, imeandikwa nitakwenda mbele yako na kupasawazisha pale palipo paruza kwa jina la Yesu, Nisafisha njia zangu za mafanikio kwa jina la Yesu. Napanda kuwa wa juu kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu maana imeandikwa utakuwa kichwa na wala si mkia. Nakataa kuwa mkia kwa jina la Yesu. Bali najitamkia mafanikio juu ya maisha yangu kwa jina la Yesu.

by Information Ministry

usikose kufuatilia mwendelezo wa masomo mengine ya ufufuo na uzima Arusha yanayo fundishwa na askofu Frank Andrea au ungana nasi live kupitia link :-
·        
·                                                                    
·