IBADA YA TAREHE 17/08/2014
SOMO: SHETANI KATIKA UZAO WA WANADAMU
MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima |
Shetani ni roho lakini alishahama katika roho na yupo
katikati ya wanadamu na unaweza kumkuta mtu anaonekana binadamu kumbe ana roho
ya kishetani. Mafarisayo walipomwendea
Yesu katika Mathayo23:33 Yesu aliwaambia 33 Enyi
nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? pia katika kitabu cha Mathayo 12:34 34 Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya?
Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu
mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.
pia kitabu cha Mwanzo 3:15 15 nami nitaweka
uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo
utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigin. Kwa ufupi kuna wanadamu kabisa
tunaishi nao lakini si binadamu kama wanavyoonekana kwa jinsi ya mwili.
Mwanzo19:1-10 Basi, wale malaika
wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu
akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie
nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na
mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake.
Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. 4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma,
wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.
5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu
waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
Lutu alikuwa anaongea na hawa malaika ili wale na wanawe
miguu wakati ni malaika na hakujua kama ni malaika, lakini sio watu, malaika
hawa Lutu amewaona kana kwamba ni binadamu na walikula chakula na hii
inatufundisha kumbe sio kila anayekula umwite mtu lazima ujue kuna uzao usio wa
kibinadamu unafanya kazi pamoja na wanadamu na kazi Yetu ni kuuondoa ule
uzao na kujenga Ufalme wa mwanakondoo.
Hata wale wenyeji wa mji wa sodoma na gomora waliwadhania kuwa ni watu lakini
walikuwa ni malaika.
Waebrania13:2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine
wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
Hapa tunajifunza kuwa tunaweza kukutana na mtu njiani na
kumfadhili kumbe ni malaika wa giza aliye vaa mwili na tunatakiwa tuangalie
zaidi ya akili za kibinadamu ili kujua aliye mtu na asiye mtu, sio unakutana na
mtu njiani anakuambia anakupenda hapohapo mnachukuana na kwenda nyumbani na
baadae mnafunga ndoa na matatizo yanakujia tangu ulipoanza uhusiano na mtu huyo
ama wa kibiashara au kimwili lakini kiuhalisia yule alikua ni uzao wa kishetani
aliye kuja kwako na kukuletea matatizo.
Kuna binadamu lakini ni mashetani asilimia miamoja
wamejichanganya katika uzao wa wanadamu na kufanya mambo ya ajabu lakini
wanaonekana ni watu wa kawaida tu kumbe ni mashetani wametumwa toka kuzimu kuja
duniani kuharibu mataifa na maisha ya watu. Majini,majoka,mizimu,miungu ya
mashariki ya mbali, mapepo wanaitwa malaika wachafu(waovu) wote hao wanaweza
kuvaa mwili na kuishi na binadamu makazi yao ni kuzimu ndio hao Biblia
inawaongelea kwamba “ni rahisi kueneza
mambo machafu na wanahekima kwa mambo mabaya lakini ni wapuuzi kwa mambo yalio
mema” na hao wataangamizwa kwa jina la Yesu. Na malaika wema ni malaika
watakatifu wanakaa mbinguni. Malaika wote wanaweza kujigeuza kuwa kitu
chochote.
Waebrania1: 7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake
kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
Malaika wetu wa mbinguni wanaweza kugeuka kuwa upepo
Yuda1: 6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini
wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya
giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Hawa ni mashetani lakini ni malaika wagiza.
Ufunuo12: 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake
wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
Uzao wa kishetani katikati ya wanadamu na nyakati hizi ni
nyakati ambazo mpinga kristo anataka kuingia duniani na atakuwa na mama yake na
Baba yake lakini watu hawajui hili kwakua wanajua kila aliye na mwili ni
mwanadamu wa kawaida Mfano Yesu alikuwa anajulikana ni mwana wa Yusufu na
Mariamu kumbe alikuwa katoka Mbinguni kwenye makao yake na ni mwana wa Mungu
Baba wa mbinguni.
Yesu alikutana na mwanamke mmoja kisimani na Yesu alimuuliza
kuwa unaye mume? Yule mama alimjibu hapana maana nilio nao ni watano na akajibu
sina mume na Yesu akasema umesema vyema, maana yake alikuwa na wanaume ambao
wanamharibia maisha yake.
Biblia inasema mpingeni shetani naye atawakimbia na
hatutakiwi kuwakimbia watu hawa wenye miili ya kibinadamu waliotoka kuzimu bali
tunawafuata huko huko walipo. Na huyu jini au joka anaweza kuwa Mchungaji, Mwanasiasa,
Paroko, au mtu yeyote anaongea vizuri lakini sio mtu anamwili wa kibinadamu ndani
anaroho ya kishetani.
Namna ambayo hawa mashetani watu wanaweza kumwangamiza mtu
1.
Kwa njia ya macho, mtu anaweza kukuangalia tu
ukauua wiki mbili. Kwa kutumia macho yako anakurushia vitu na vinakupata.
2.
Kupitia mahusihano ya kimwili
“1Wakorintho6: 16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili
mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.” Biblia inasema mume
na mke wanapooana wanakua na uhusihano na uhusihano unaewaleta pamoja na aliye
umbwa na kahaba ni mwili mmoja . pia Yesu kristo na sisi kanisa tunauhusiano
kupitia Roho mtakatifu. Shetani anapokuwa na uhusihanowa kimwili na mtu lengo
lao ni kuwawekea watu matatizo unashangaa bihashara inaanza kuharibika au
unashangaa unapatwa na mikosi kumbe ni unakua umejiungamanisha na shetani
uliyefanya naye mahusihano. Pia kwenya ndoto unapoota unafanya mahusihano unakuwa
unajiungamanisha na mashetani na hapo matatizo yanakua yanaanza na ukifuatilia
maisha yako unaona matatizo yako yameanzia pale ulipokutana kimwili na mtu
Fulani ambaye ndani yake anakusudi la kishetani. Pia unapoona mtu anajiuza unadhani ni mtu kumbe
ni shetani yupo mawindoni na anapokutana na mtu kimwili anamwachia ushetani
ndani yake na mambo yake yanaanza kuharibika na anakua anamilikiwa na nguvu ya
kishetani kwenye maisha yake ma mambo yanaanza kuharibika.
ZABURI 78:49 Akawapelekea ukali wa hasira yake, Ghadhabu, na uchungu, na
taabu, Kundi la malaika waletao mabaya.
3.
Kupokea zawadi kutoka kwake. Nguvu inaweza kuwa
ndani ya kitu ulichopewa na mtu
Matendo ya mitume19: 12 hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini
mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. Maana yake kile
kinachotoka kwa mtumishi wa Bwana kinabeba uweza wa Bwana na kinaweza kutenda
miujiza kwa wagonjwa. Sasa vilevile na mashetani wanaweza wakabeba uweza wa
kishetani kwenye vitu na matatizo yakawapata watu mfano mikufu, saa, nguo
viatu,gari, au kitu chochote kinakuwa kimebeba uweza wa kishetani ndani yake kama magonjwa na matatozi mengine”
kwa jina la yesu ninaangamiza chochote nilichopewa kama zawadi au nimenunua
mimi mwenyewe, kwa jina la Yesu chochote kile kilichopandwa ili kuharibu
familia au kazi yangu kama ni kitambaa nakuamuru uteketee, kama ni zawadi
nakutetekeza kwa damu ya Mwana Kondoo
ushetani ulioletwa kwa njia ya macho au kwa njia ya zawadi ya aina
yeyote naiteketeza kwa jina la Yesu, nateketeza kwa jina la Yesu(unapoomba hivi
kwenye ulimwengu wa Roho vinateketea) kwa jina la Yesu naiteketeza kila zawadi
niliyopewa na mtu yeyote asiye binadamu aliyekuja kwenye maisha yangu namteketeza
kwa jina la Yesu, iwe ni zawadi iliyonuiziwa kifo, balaa, mikosi, naivunja kwa
jina la Yesu, kitu chochote kilichonuiziwa manuizo ya kishetani juu yangu au familia yangu nakiteketeza kwa
damu ya mwana kondoo. Namshambulia binadamu yeyote aliyetumwa kuja kufanya
mahusihano na mimi na kuniwekea manuizo ya kishetani namshaambulia kwa jina la
Yesu, kwa damu ya mwanakondoo, aliyenitupia mishale kwa njia ya macho, chakula, maji ninaiharibu
kwa damu ya mwanakondoo, kwa jina la Yesu ushetani wowote uliotumwa ndani yangu
naukataa kwa jina la Yesu. Jini wa
uchawi aliye tumwa kwangu kwa njia ya kishetani na balaa na mikosi iliyopangwa
juu yangu naivunja kwa jina la Yessu na kifo kilichopangwa juu yangu nakifuta
kwa damu ya mwanakondoo. Sitakufa kwa jina la Yesu, kifo chochote kilichopangwa
juu yangu nakivunja kwa jina la yesu. Navunja
tamaduni zote za kishetani kwa jina la
Yesu.
AMEN.
No comments:
Post a Comment