UTANGULIZI
Isaya 45:1-3
Mungu anasema
nitakwenda mbele yako naminitakupa hazina za gizana na mali zilizo fichwa za
mahali pa siri. Kuna vitu vipo vimefichwa za mahari pa siri ambavyo Bwana
anahaidi atatupatia, Ni muhimu kujua kunavitu vipo ambavyo havionekani lakini
Mungu amekuandalia wewe. Hata wakati wa uumbaji kunavitu Mungu alkuwa anavitaja
lakini havikuako, Mwanzo 1:1-2, Mungu aliumba dunia na vyote kwa Neno. Kwa
maneno mengine ukivichukua vitu vyote na kuviludisha viliko toka vitarudi ndani
ya Neno la Mungu. Kitabu cha Yohana 1:1-5 kinasema vitu vyote viliubwa kwa Neno
na Ndani ya huyo Neno ndimo mlimokuwepo uzima,,
Neno ni nini?
Kwenye maandiko
Matakatifu yaani Bilblia emeeleza Neno kwa namna mbili
i.
YESU
ii.
MBEGU
NENO KWA MAANA YA YESU
YESU ni Neno
Yohana1:1-4. Neno lilikuwa kinywani mwa MUNGU. Ukikusanya vituvyote virudi
kwenye hasiri yake vyote vitarudi kwenye Neno. Huyu Neno kazi yake ilikuwa ni
kumtia nuru kila mmoja ulimwenguni. Yohana1:14 inasema naye Neno akavaa mwili
tukauona utukufu wake kama wa mwana pekee wa Mungu ambaye alikuwa ni Yesu.
NENO KWA MAANA YA MBEGU
Kitabu Luka 8:11
kinaeleza vizuri kuwa mbegu ni Neno la Mungu. kwa maneno mengine unaweza kusema
ndani ya Mbegu ndimo mlimokuwepo uzima. Kwa mfano ukiwa na mbegu ya parachichi ndani
yake kuna mapori ya maparachichi. Ukiwa na mbegu ya mchungwa ndani yake kuna
mapori ya michungwa. Iliuendane na Mungu lazima ujifunze kuona kama yeye anavyoona..
Utaona Yesu anatoa mfano
wa mbegu Luka 8:4-8, Yesu alikuwa anazungumzia Mbegu kama neno la Mungu na
mahari pa kupanda kama aina za mioyo ya watu ambao wanalisikia Neno la
Mungu. Aina za mahari pa kupanda mbegu
i.
Njiani : moyo njia ni moyo ambao mtu
analisikia Neno la Mungu lakini anafungua
moyo wake na kuruhusu mambo mabaya kuingia kwake. Na ndege huja kuula
ii.
Mwamba: moyo mwamba ni moyo usio tayari
kupokea chochote, ulisikiliza Neno lakini hulizuia lisiingie ndani yake.
iii.
Udongo wa Miiba: moyo miiba ni moyo
buzy, moyo ambao unasongwa na mambo mengi ya duniani, kama kazi, maisha n.k
iv.
Udongo mzuri:mbegu iliyo dondoka kwenye
udongo mzuri, ni mbegu ambayo imeanguka kwenye moyo mzuri ambao upo tayari
kulipokea neno la Mungu na kulitendea kazi, hasa kuzaa watu katika ufalme wa
Mungu.
Kunamambo mengina Unaweza
kupanda kwa roho yako na kwa mwili;- kuna vitu unavipata au unapanda katika
roho unapo sikiliza Neno la Mungu. Kupanda kwa mwili;- kunamatendo ya mwili
unayafanya ambayo hayana faida kwenye roho yako. mwanzo 2:7 mwili wa mwana damu
ni mavumbi ya aridhi kwa maana yake unaweza kupanda jambo na likaota kwenye
mwili. Ndio maana Mungu alimwambia shetani utakula mavimbi ya ardhi ndio maana
ni rahisi kwa shetani kupanda magonjwa kwenye mwili wako.
Mwanzo1:12 miche na
itoe mbegu, ambazo mbegu zake zimo ndani. Maana yake ndani ya mbegu moja kuna
mapori. Mfano mzuri utaona kwa wakulima wanapanda mbegu moja lakini wana vuna
muhindi ambao unapunje elfu moja. Je mtu angekula ile punje ya muhindi, maana
yake amekula magunia ya mahindi.
MFANO WA MTUNZA MBEGU
KAMA NENO LA MUNGU
Utaona
katika Biblia kuna watu ambao Mungu aliwajua toka tumboni na kumwambia Raheli
mataifa makubwa mawili yanapigana ndani yako. Mwanzo 25:21- 34 mataifa mawili
ndani ya tumbo moja, baadaye walizaliwa kwake watoto mapacha, Yakobo na Essau.
Yakobo alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anatunza mbegu. Lakini Esau alikuwa ni
mwindaji na alikuwa hana uwezo wa kuifazi mbegu, kwasababu alikuwa akiwinda kwa mshale na kummaliza
mnyama. Yakobo alikuwa mkulima ndio maana alikuwa ana tunza mbegu. Utaona
kwenye maandiko Essau aliamua kuuza uzaliwa wake wa kwanza kwasababu alikuwa
atunzi mbegu kwenye ghala yake. Hakasahau kuwa kuna Baraka ya kuwa mzariwa wa
kwanza. Kwenye Biblia kuna Baraka nyingi
za mzariwa wa kwanza lakini kubwa ni hizi:-
BARAKA
YA MZALIWA WA KWANZA
i.
Baraka ya mzazi
ii.
Baraka ya Mungu: Mungu anasema mtoto wa
kwanza ni wa Kwangu.
iii.
Ni mtawala wa familia.
Hatakama umezaliwa
maskini ila kwa Baraka za Mungu utafanikiwa.
Essau na Yakobo nani
alikuwa Mwizi?
Essau alimwambia Yakobo
umeniibia Baraka zangu za uzaliwa wa kwanza, amesahau kwamba alimuuzia uzaliwa
wake wa kwanza kwa Yakobo. Kwa maneno mengine kwenye ulimwengu waroho Yakobo
alikuwa Essau na Essau alikuwa ni Yakobo. Ndio maana kila mahari Yakobo alipo
kwenda alifanikiwa, alipo kuwa kwa Labani alipokuwa anafuga wanyama na
wakazaliana sana. Siri ya Yakobo alikuwa anatunza mbegu.
MANENO KAMA MBEGU
Neno la Mungu ni mbegu.
Hata maneno ya shetani ni mbegu. Kuna maneno ambayo unajitamkia mwenyewe mabaya
yanakuwa ni mbegu kwenye maisha yako. Ndio maana akasema kwenye kitabu cha
Yoeri aliye zaifu na aseme mimi ni hodari.
Kanuni ya mbegu ni
lazima ioze kabla haija tokea. Maandiko yanasema mbegu isipo anguka chini ya
aridhi ikafa haiwezi kumea. Unapo panda mbegu kuna kipindi cha kuishi kwa
imani. Kwa mfano ukipanda karanga na kufukia, watu hawata jua hatakama Utaendelea
kumwagilia kwasababu ipo chini ya aridhi, lakini unapo zidi kumwagiria ndipo utakapo
una imetokea au kuchanua. Lakini wapo wengine wakimwagia wasipoona kitu na hukata
tamaa kwa sababu hajaona kitu kinacho onekana pale. Unapo panda mbegu kanuni ya
imani inaanza kutumika. Nikama mchungaji akisema poke Biashara kubwa, uanze
kuona umepokea kama mbegu. Na uanze kutengeneza picha na kumshukuru BWANA na
BWANA atakuinua 2wakorintho4:7 utu wetu wanje unachakaa la kini wa ndani
unafanywa upya siku kwa siku. Ishi kwa imani leo ilikesho ukavune. Kunawatu
wanakuzalau leo ilakesho watakueshimu kwa jina la YESU. Muhubiri 11:1-6,
paangukiapo ule mti papohapo utalala; imani yako inaangukia wapi? Sitakufa bali
nitaishi, anasema asubuhi panda wala
usiuzuie mkono wako, wewe panda kila unachokiona baada ya muda utakiona kile
ulicho kipanda. Asubuhi panda, jioni panda, usiku panda. Panda kwenye uongozi,
utajiri, mifugo, mali na hazina. Unapokuwa na mbegu usione kama umeshika mbegu
ona kama umebeba mapori ya iyo mbegu. Muhubiri 4:14
Unapo panda ukiona mche
umetokea anza kuweka na walinzi wa kulinda maana biashara yako, kazi yako,
maisha yako yanaenda kuwa mti mkubwa. Kama unacheleani moja anzakuona unachuo
cha ushonaji. BWANA akamwambia Abrahimu inua macho yako kuanzia hapo ulipo nchi
uonayo nimekupa. Mungu anataka kukutoa kutokea hapo ulipo,, hauwezikuishia hapo
kwa jina la Yesu anza kuona ushindi mbele yako kwa Jina la Yesu. Je unaona nini
mbele yako leo? Unaona mbegu au unaona pori? Unambegu ndani yako Mungu kaiweka
unatakiwa uimwagilie kwa jina la Yesu. Mungu anasema inua macho yako tazama
kutokea hapo ulipo anza kuangalia unapo kwenda kwa jina la Yesu
Watu wanapo kuona maisha yako wana comment maisha
yako unayo ishi leo, lakini Bwana anampango mpya na wewe. Heri apandaye kwa
machozi atavuna kwa furaha.
Maombi
Baba Mungu katika jina
la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai,Napanda ushindi juu ya maisha yangu kwa
jina la Yesu, imeandikwa nitakwenda mbele yako na kupasawazisha pale palipo
paruza kwa jina la Yesu, Nisafisha njia zangu za mafanikio kwa jina la Yesu.
Napanda kuwa wa juu kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu maana imeandikwa
utakuwa kichwa na wala si mkia. Nakataa kuwa mkia kwa jina la Yesu. Bali
najitamkia mafanikio juu ya maisha yangu kwa jina la Yesu.
by Information Ministry
usikose kufuatilia mwendelezo wa masomo mengine ya ufufuo na uzima Arusha yanayo fundishwa na askofu Frank Andrea au ungana nasi live kupitia link :-
·